26 May 2022, 9:49 am
RUNGWE-MBEYA
NA:LETHISIA SHIMBI
Jamii wilayani Rungwe mkoani Mbeya imetakiwa kuachana na mtazamo hasi kuhusu watu wenye ulemavu badala yake wametakiwa kujumuika kwa pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali.
Rai hiyo imetolewa na Meneja wa shirika la TRAIDCRAFT EXCHARGE Ndg Ledis Kigala kwenye mkutano na wananchi uliofanyika katika ofisi za CCM kijiji cha Nsongola kata ya Bujela ambapo amesema kuwa watu wenye ulemavu wamekuwa wakibaguliwa katika jamii kitendo ambacho kinapelekea watu hao kukosa sauti katika jamii.
Aidha amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakitumia majina yasiyostahili kuwaita watu wenye ulemavu kwa mfano kipofu ,zeruzeru,badala ya kusema mtu asiyeona ,au albino.
naye mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu(CHAWATA) Ndg EMU KASOKE ameitaka jamii kutokuwa na tabia za kuwatenga bali kuwapa nafasi katika jamii na wana haki kama watu wengine.
kwa upande VERONIKA DANIEL Afisa usitawi wa jamii wilayani Rungwe amekemea vikali kitendo cha ubaguzi kwa watu wenye ulemavu na amesema kuwa endapo itabainika jamii au mzazi anambagua mtu mwenye ulemavu na kutompa haki yake jamii itoe taarifa kwenye ofisi za ustawi na jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia ili hatua kali zichukuliwe
TRAIDCRAFT EXCHARGE ni shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na mambo mbalimbali ikiwemo kuelimisha jamii juu ya kubadilisha mitazamo hasi kwa watu wenye ulemavu.