Wafanyabiashara 1800 Rungwe wanufaika na mafunzo.
25 May 2022, 10:24 am
RUNGWE-MBEYA
NA:BETRIDA ANYEGILE
Wafanyabiashara elfu moja na mia nane kutoka kata takribani kumi Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wamepatiwa mafunzo ya urasimishaji biashara na Mpango wa kurasimisha rasirimali na biashara Tanzania ( MKURABITA).
Akizungumza na vyombo vya habari katika kufunga mafunzo kwenye Kata ya Kiwira Wilayani Rungwe Mkurugenzi wa Mkurabita Tanzania bi Jane Lyimo amesema mafunzo yalikuwa na muitiko mkubwa kwa wafanyabiashara kutoka kada mbalimbali wameonesha nia ya kurasimisha biashara zao kuwa rasmi.
Bi Lyimo amesema mafunzo yamehamasisha wafanyabiashara kutaka kupata mikopo kutoka taasisi za fedha kwa kuanza hatua za awali kujisajili,kufungua akaunti za benki na kupata leseni kwa madereva bodaboda.
Akizungumzia changamoto zilizojitokeza wakati wa mafunzo ikiwemo elimu duni ya mikopo kwa wafanyabiashara na baadhi ya bodaboda kukosa leseni hali inayopelekea kukosa fursa mbalimbali zinazojitokeza.
Mafunzo ya kurasimisha rasirimali na biashara Wilayani Rungwe yamefanyika katika Kata ya Makandana,Kawetele,Bulyaga,Bagamoyo,Ibighi,Kyimo,Isongole,Mpuguso na Kiwira huku yakiudhuliwa na taasisi mbalimbali Wilayani hapa.