Mkurabita awa Mkombozi kwa wafanyabiashara
19 May 2022, 2:22 pm
Wafanyabiashara Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wametakiwa kurasimisha shughuli zao za biashara ili kupanua wigo wa kuzifikia fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na urahisi wa kupata mikopo na leseni za biashara.
Hayo yamejiri katika ufunguzi wa mafunzo ya kurasimisha biashara za kawaida na Bodaboda yaliyoshirikisha wafanyabiashara kutoka Kata ya Kawetele,Makandana,Bulyaga na Bagamoyo katika ukumbi wa Halmashauri wa Mwankenja.
Katika ufunguzi huo mgeni rasmi mh Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Dkt Vicent Anney amesema mafunzo hayo yawe na matokeo kwa kukuza biashara na kuunganishwa na masoko ndani na nje ya nchi.
Aidha Dkt Anney amesema kurasimisha wafanyabiasha kutasaidia wafanyabishara kulipa kodi kwa Serikali hali iatakayosaidia kuongeza pato la taifa.
Naye mkurugenzi wa urasimishaji Ardhi na Biashara bi Jane Lyimo amesema katika kuwafikia wafanyabishara Mhe. Rais ameleta MKURABITA na kupatia fedha zilizosaidia ujenzi wa kituo cha huduma kwa pamoja katika eneo la Mamlaka ya Mji mdogo Tukuyu.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo bi Joyce Mkumbwa na ndugu Imani Mwangupi wameishukuru serikali kwa kuwaona wafanyabiashara na kuwaletea Mkurabita ili waweze kurasimisha biashara zao na kuweza kupata mikopo inayotolewa na taasisi za fedha.