Watumiaji wa vyombo vya moto wametakiwa kujua umuhimu wa fidia ya bima
8 April 2022, 7:43 am
RUNGWE-MBEYA
Watumiaji wa vyombo vya moto wametakiwa kujua umuhimu wa fidia ya bima ya gari baada ya kupata ajali ilikuweza kupata fidia pindi apatapo matibabu.
Hayo yamejiri baada ya mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wilaya ya Rungwe Felix Kakolanya wakati akizungumza katika kipindi chai fm redio ambapo amesema kuwa kuna aina mbili za bima ya gari kubwa na bima ya tatu ambapo zote mbili zinategemeana .
.
Kakolanya amebainisha vigezo ambavyo abiria anatakiwa kufuata pindi anahitaji bima hiyo kuwa ni pamoja na kuandika barua kwenda kwa kampuni husika ikiambatana na fomu ya polisi na tiketi ya gari
.
Aidha ameongeza kuwa kuna mfumo kwa hivi sasa wa kielektroniki ambapo abiria anaweza kuangalia kama gari alililopanda lina bima hali itakayosaidia waendesha vyombo vya moto kuweka bima mahali ambapo kila abiria anaweza kuiona pindi apandapo gari hiyo.
.
Hata hivyo amemaliza kwa kuwataka wasafiri kutoa taarifa endapo dereva anakwenda kwa mwendo kasi kuepukana na ajali zinazoweza epukika.
.