Jamii itoe taarifa vitendo vya ukatili kwenye madawati
3 April 2022, 6:24 am
RUNGWE-MBEYA
Taasisi isiyo ya kiserikali inayotekeleza mradi wa mwanamke imara WiLDAF imetaka jamii kutoa taarifa kwenye madawati ya kijinsia pindi vitendo vya ukatili vinapojitokeza katika jamii.
kauli hiyo imetolewa wana Mwanasheria SUZAN KAWANGA pamoja na mwelimishaji Ndg THOMAS MPONDA waliopokuwa wakitoa elimu kwa njia ya radio Chai FM huku wakisema kuwa jamii inapaswa kuwa karibu na watoto katika malezi ili kuweza kupata taarifa kwa watoto
Kwa upande wake thomas mponda alianza kwa kuelezea maana ya ukatili na ukatili wa kijinsia
kwa upande mwingine THOMAS MPONDA amewaomba wanaume kutoa taarifa kwenye vyombo na madawati pale wanapofanyiwa vitendo vya ukatili na kutaka jamii kuacha vitende vya ukatili.
hata hivyo Mwanasheria SUZAN KAWANGA ameiomba jamii kutoa ushirikiano kwenye vyombo vinavyo sikiliza kesi kwani kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watu kushindwa kutoa ushirikiano na kesi kumalizwa kienyeji.