Kamati ya Bunge ya uongozi ya serikali za mitaa [TAMISEMI ] yaridhishwa ujenzi wa barabara Rungwe
16 March 2022, 10:41 am
RUNGWE
Na Lennox Mwamakula
Kamati ya Bunge ya uongozi ya serikali za mitaa [TAMISEMI ] imefanya ziara wilayani Rungwe mkoani Mbeya ya ukaguzi wa barabara ya kutoka Masebe-Bugoba hadi Lutete yenye urefu wa kilometa 12 iliyo jengwa kwa kiwango cha lami na kuridhishwa na ujenzi huo.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa barabara hiyo mhandisi wa tarura mkoa wa Mbeya Wilson Charles amesema uwepo wa barabara hiyo kumewarahisishia wananchi waishio maeneo hayo kusafirisha mazao yao kwa urahisi kwani kumekuwa na ongezeko kubwa la uzalishaji wa mazao ya biashara.
Akipokea taarifa hiyo mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Abdallar Chaulio ameupongeza uongozi wa mkoa wa mbeya kwa ushirikiaano mzuri wanao uonyesha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na amewaomba mameneja wa TARUA wa wilayani kuwashirikisha wabunge ili kuweza kusaidiana pale panakuwa na changamoto
Kwa upande wake Waziri wa Nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na Serikali za mitaa [TAMISEMI] Mh, Innocent Bashungwa ameishukuru kamati hiyo kwa kuridhishwa na ujenzi wa barabara hiyo na kuiomba kamati hiyo kuona namna ya kuwepo kwa ushirikiano baina ya TANROADS na TARURA ili kuweza kukamilisha kipande cha barabara cha kutoka ushirika Mjini hadi Masebe chenye urefu wa kilometa moja ambacho kipo chini ya TANROADS
Naye mkuu wa mkoa wa mbeya mh, Juma Homera amesema kuwa barabara zote zinazo jengwa ofisi ya mkuu wa mkoa imetoa maagizo kufungwa taa za barabarani ili wanachi waweze kutumia barabara hizo kwa yakati zote