Chai FM

Ubovu wa barabara kikwazo katika maendeleo

22 February 2022, 8:41 am

RUNGWE -MBEYA

Wafanyabiashara pamoja na wakazi wa kijiji cha Mpandapanda kilichopo kata ya Kiwira wilayani Rungwe ambapo wameeleza namna wanavyoshindwa kufanya maendeleo ya kiuchumi kutokana na uharibifu wa miundombinu ya barabara.

wakibainisha hayo baadhi ya wakazi pamoja na  wafanyabiashara wamesema kuwa kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara inapelekea wao kushindwa kufanya kazi za kuichumi pamoja na kushindwa kusafirisha bidhaa zao pindi wanapotaka kuzifikisha sokoni.

Pia wameeleza namana hali hiyo inavyowaathiri ikiwa ni  kutumia gharama kubwa katika usafirishaji wa mazao yao kuyafikisha sokoni  kwani  inawalazimu kupita njia ya mzunguko na wameiomba serikali iwasaidie kuboresha miundombinu hiyo.

Kwa upande wao nao bodaboda ambao ni miongoni mwa watumiaji wa barabara hiyo wameeleza changamoto wanazokumbana nazo kutokana na miundombinu mibovu ya barabara hiyo ikiwa ni pamoja na kutumia mafuta mengi kwani inawalazimu kutafuta njia ya mzunguko ili  kulinda maisha ya abiria.

Sanjari na hayo kupitia changamoto za wakazi hao chai fm imeweza kuongea na IPIYANA ELIUD ambaye ni mwenyekiti wa kijiji hicho ili kujua mapango mkakati wa kukarabati barabara hiyo amabapo  amesema kuwa barabara hiyo tayari  ipo kwenye harakati za matengenezo na kufikia apirl itakuwa tayari kwani tayari ipo kwenye mikono ya TARURA kwa ajiri ya matengenezo.