Malezi mabaya kwa watoto chanzo cha matukio ya uhalifu
21 February 2022, 8:14 am
RUNGWE-MBEYA
Malezi mabaya kwa watoto wilayani Rungwe Mkoani Mbeya imeelezwa kuwa chanzo cha matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia na mauaji.
Ameyasema hayo Mch wa kanisa la Baptist Tukuyu mjini Mch. .HALLENCE MWASOMOLA, wakati akizungumza na redio chai fm ambapo amesema uwepo wa malezi mabaya kwa watoto inaweza ikapelekea vitendo vya kihalifu kwani watoto wengi wamekuwa wakifanya vitu kutokana na malezi ya wazazi wao.
Aidha Mwasomola ameongeza kwa kuiomba jamii kuto kujihusisha na vitendo vyote vya kihalifu kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi na kupelekea uvunjifu wa amani ambayo ni tunu ambayo tunatakiwa kuilinda.
Kwa upande wake Mrakibu mwandamizi mkuu wa Polisi wilaya ya Rungwe PHILIPO MHAKO, amewashukuru wakazi wilayani hapa kwa ushirikiano mkubwa wanao endelea kuuonesha na kupelekea kuwabaini wahalifu wote wanao jihusisha na vitendo hivyo katika jamii.
Sanjali na hayo MHAKO, amewaomba wananchi pindi wanapo toa taarifa juu ya vitendo vya kihalifu pia wasisite kutoa ushirikiano wa ushahidi wa vitendo hivyo pale wanapo wabaini wahalifu kwani kufanya hivyo kutafanya kivitokomeza kabisa vitendo vyote vya kihalifu katika jamii.
BETY MWAMBESO na OLIMPA MBETE, ni wananchi wilayani hapa wameiomba jamii kuwa na hofu ya Mungu kwa kuto kujihusisha na vitendo vya kikatili, na malezi mabaya kwa watoto kwa kuto kuwaruhusu watoto kufanya vitendo vyote ambavyo ni kinyume na maadili ikiwemo matumizi ya simu kwa watoto.