Wauguzi wajengewa uwezo kuhusu mdomo Sungura
10 February 2022, 12:10 pm
MBEYA
Mafunzo ya siku tatu kuwajengea uwezo wauguzi wa hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya yameanza rasmi ili kukabiliana na watoto wanaozaliwa mdomo wazi na mdomo sungura ili waweze kupatiwa matibabu mapema.
Dkt Zackaria Amos ni Mkufunzi wa mafunzo hayo anaeleza lengo la mafunzo
Kwa upande wake meneja wa mradi kutoka shirika la Smile Veronica Kamwela amesema mafunzo hayo ya siku tatu yatawasaidia wauguzi kupata mbinu bora za kuwasaidia watoto wawapo katika matibabu.
Naye muuguzi mkuu hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya Petro Seme amepata fursa ya kutoa neno kwa wauguzi na wakufunzi.
Tatizo la mdomo wazi na mdomo sungura limekuwa kubwa nchini na wengi wa wazazi huwaficha watoto hao ndani kwa kile walichodai ni mkosi ambapo sasa huduma ya urekebishaji hufanyika bure kwa ufanisi mkubwa hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya huku elimu ikiendelea kutolewa kwa wananchi.