Waandishi wawe chachu elimu dhidi ya vitendo vya ukatili
8 February 2022, 5:58 pm
MBEYA
Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Kaimu Afisa Elimu Mkoa Wilbrod Yanga amewataka Waandishi wa habari chipukizi ishirini na moja Mkoani Mbeya walionufaika na mradi wa SAUTI MPYA kuendeleza elimu waliyoipata baada ya mradi huo wa miaka miwili kumalizika chini ya ufadhili wa shirika la We World.
Yanga ameyasema hayo Jijini Mbeya katika mkutano wa meza ya duara ukijumuisha waandishi chipukizi,asasi za kiraia,viongozi wa serikali na waandishi waandamizi kutoka vyombo
Kwa upande wake Zamda Mafimba Mratibu wa mradi We World Mkoa wa Mbeya anaeleza lengo la mradi kwa waandishi chipukizi
Naye Mratibu wa KIWOHEDE Mkoa wa Mbeya Baraka Masatu amesema mbali ya mafunzo kwa waandishi wa habari pia wametoa elimu kwa jamii…
Baadhi ya waandishi walionufaika na mafunzo hayo wanaeleza changamoto zinazowakabili waandishi pindi wakitekeleza majukumu yao
Mradi wa SAUTI MPYA umepata mafanikio makubwa mbali ya waandishi kuibua mambo mbalimbali katika jamii nao wananchi wengi wamejitokeza kuainisha vitendo vya ukatili vinavyoashiria uvunjifu wa haki za binadamu.