Wizi wa pikipiki wakwamisha ndoto za vijana
2 February 2022, 6:01 am
RUNGWE-MBEYA
Wananchi wa kata ya kawetele wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwa pamoja wameadhimia kuunda mpango wa pamoja wa kuanzisha ulinzi shirikishi (sungusungu) ndani ya kata hiyo kutokana na videndo vya wizi vinavyoendelea.
kauli hiyo ya kuadhimia imekuja kwenye mkutano ulioitishwa na mwenyekiti wa kijiji cha kawetele chini ALPHONCE MWABULAMBO kutokana na baadhi ya vijana wa bodaboda kuibiwa pikipiki zao ndani ya kata hiyo na kupeleka malalamiko yao kwa mwenyekiti huyo.
mwenyekiti wa kijiji hicho cha Kawetele chini amesema changamoto iliyopo ndani kijiji na kata kwa ujumla ni kwa baadhi ya mwenye nyumba kuwapangishia watu nyumba bila kujua taarifa za mtu alikotoka huku akiwaomba wenye nyumba kuwa na utaratibu wa kumtambulisha mpangaji kwa serikali ya kijiji.
kwa upande wao wananchi walioudhuria kwenye mkutano huo wamemuomba mwenyekiti kuwa na utaratibu wa kuhitisha mikutano mara kwa mara ili kuweza kuwabaini watu wasio itakia mema kata hiyo ya Kawetele
aidha nao waendesha pikipiki hizo maarufu kama bodaboda wamesikishwa na vitendo vya wizi vinavyo endelea ndani ya kata hiyo Kwani vimekuwa vikiwazua vijana kuinuka kiuchumi kwani kupitia usafirisha imekuwa kazi ambayo imeajiri vijana wengi katika jamii na kuomba ushirikiano kwa jamii.