Abiria watoe taarifa kuepusha ajali barabarani
27 January 2022, 6:58 am
RUNGWE-MBEYA
Tabia za kibinadamu zimepelekea kuongezeka kwa ajali barabarani kote nchini hadi kufikia asilimia 76% kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa hivi karibuni na jeshi la polisi.
Akizungumza na Radio cha FM kupitia kipindi cha Amka na Chai Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani wilayani Rungwe Felix Kakolanya amesema tabia za kibinadamu kama kutoheshimu sheria za usalama barabarani zimekua zikipelekea ajali kuongezeka.
Akizungumzia umuhimu wa tiketi kwa abiria Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Rungwe Felix Kakolanya amesema abiria wawe na utaratibu wa kutunza tiketi huku akiwataka abiria kutoa taarifa kwa polisi usalama barabarani pale ambapo dereva anakihuka sheria na kuhatarisha usalama barabarani.
Ameongeza kuwa abiria wa umuhimu mkubwa katika kuzuia ajali barabarani hivyo wanawajibu kuchukua tahadhari kwa kutokubali kupakiwa wengi katika gari na kutokubali kuendeshwa kwa mwendokasi hali itakayohatarisha usalama na kupelekea ajali.