Madarasa 24 yakamilikika kwa asilimia 100
3 January 2022, 9:46 am
RUNGWE-MBEYA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Busokelo Bi, LOEMA PETER amekabidhi takribani vyumba vya madarasa 24 kwa Mkuu wa wilaya ya Rungwe baada ya kumalika ndani ya muda ulio pangwa.
Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na kituo hiki huku akieleza kuwa makabidhiano yamefanyika december 30 mwaka 2021 na kusema vyumba hivyo vimekamilika kwa asilimia mia moja na kila chumba kikiwa na madawati kwa maandalizi ya muhula wa masomo januari 2022.
Hata hivyo Bi LOEMA amesema kutokana na fedha hizo za ujenzi wa vyumba vya madarasa,kama halmashauri ya Busokeko katika ujenzi huo wamejenga ofisi za walimu ili kuwaondolea adha walimu ya kutumia chumba kimoja.
Aidha amewaomba wazazi na walezi kuwaandalia watoto sare za shule pamoja na kutoa fedha ya chakula ili wawanafunzi wawezi kusoma bila usumbufu na kuendelea kuongeza ufaulu katika shule zilizomo ndani ya halmashauri.
sanjari na hilo Mkurugenzi huyo ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, SAMIA SULUHU HASAN kwa kumuondolea mwananchi usumbufu wa kuchangia ujenzi wa madarasa kwa kutoa fedha nchi mzima kwajili ya ujenzi huo wa vyumba vya madarasa.