Wizara ya Elimu itenge fedha kwajili ya ukarabati wa shule kongwe nchini
28 November 2021, 8:37 am
RUNGWE-MBEYA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania KASSIM MAJALIWA ameagiza wizara ya Elimu kutenga fedha kwajili ya ukarabati wa shule zote kongwe nchini.
Maagizo hayo ameyatoa wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali Mkoani Mbeya wilayani Rungwe Novemba 27 mwaka huu baada ya kujionea uchakafu wa majengo kwenye shule ya sekondari ya wasichana Kayuki
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya JUMA HOMELA akimkaribisha waziri mkuu wakati wa kuweka jiwe la msingi la ufunguzi wa ujenzi wa vyumba vya mabdarasa kwa wilaya ya Rungwe amesema ujenzi wa vyumba hivyo umeanza mara moja baada ya kupokea fedha kutoka serikali kuu na ujenzi unaendelea
Aidha Waziri Mkuu majaliwa amesema serikali inaendelea kutoa fedha kwajili ya kuboresha sekta ya elimu kwaanzia ngazi ya awali hadi elimu ya juu na amefurahishwa na ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa shuleni hapo Kayuki.
Hata hivyo majaliwa amesema serikali inampango kuzikarabati shulele zote kongwe nchini ili wanafunzi wasome vizuri bila changangamoto zozote
Sambamba na hili Waziri mkuu amempongeza mkuu washule ya wasichana Kayuki wa kusimamia vizuri suala la taaluma kwa wanafunzi na kumtaka kundelea kuwa na moyo huo mzuri wa usimamiaji .