34 Wahitimu mafunzo ya Jeshi la akiba wilayani Rungwe
12 November 2021, 4:59 am
RUNGWE-MBEYA
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mh,Rashidi Chuachua amewaomba wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba [mgambo]wilayani Rungwe kuenda kuyaishi yale yote waliofundishwa wakiwa mafunzoni.
Ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya Jeshi hilo la akiba mwaka 2021 katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe amesema wahitimu wote Wahakikishe wanaenda kuwa kielelezo kwenye jamii hasa katika kupingania maslahi mapana ya taifa.
Wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi wahitimu wa mafunzo hayo AVITUS LUDOVIC na ROZI MTEWELE wameelezea changamoto mbalimbali ambazo zimewafanya kushindwa kumaliza mafunzo yao kwa baadhi ya vijana waliokuwa wamejiunga awali ikiwa ni pamoja na utovu wa nidhamu, na kuchelewa kufika kwenye mafunzo kwa mda husika.
Kwa upande wake Kepteni MOHAMED ADINANI, Akisoma changamoto walizokumbana nazo wakati wa mafunzo kwa vijana hao ni pamoja na uhaba wa vjana kujitokeza katika mafunzo hayo,pamoja na ukosefu wa bajeti ya kuendesha mafunzo hali iliyo pelekea mafunzo hayo kuendeshwa katika mazingira magumu.
Akizijibu changamoto hizo Chuachua amesema watajitahidi kwa wakati mwingine yale yaliyo jitokeza kwa mwaka huu yasijitokeze tena kwa miaka mingine na kuwaomba wahitimu kupitia vikundi vyao walivyo viunda kupitia jeshi hilo wakavitumie kujipatia mikopo isiyo kuwa na riba inayo tolewa na halmashauri.
Mafunzo hayo ya Jeshi la akiba katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe yalianzishwa mnamo tarehe 12 Julai 2021, yakiwa na wanafunzi 46 kutokana na changamoto mbalimbali jeshi limefanikiwa kuhitimishwa likiwa na vijana 34 kati yao wanawake wanne na wanaume thelasini.