Chai FM

Jamii yapaswa kuzingatia lishe kwa Watoto

31 October 2021, 4:10 am

Rungwe-Mbeya

Ili kupunguza tatizo la udumavu na utapia mlo  Jamii imetakiwa kuzingatia ulaji sahihi unaoshauriwa na wataalamu wa afya kwa watoto.

Rai hiyo imetolewa na afisa lishe wilaya ya Rungwe Bi Halima Kimeta  alipokuwa akizungumza na kituo hiki  amesema kuwa wilaya ya Rungwe ina vyakula vingi lakini bado inatatizo la udumavu hii nikutokana na kutozingazia aina ya vyakula.

Pia amewataka wajawazito kuzingatia ulaji wa chakula ili kumfanya mtoto aliye tumboni kuwa na afya bora na kuepuka kupata magonjwa mbalimbali.

Aidha Bi Halima amesema kuwa ulaji wa chakula cha aina moja ambacho hakizingatii mlo kamili, pamoja na magonjwa  vinaweza kusababisha utapiamlo.

Sanjari na hayo ameitaka jamii kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya kuanzia katika kipindi cha ujauzito, wakati wa malezi ya motto na hata watu wazima wakati wa ulaji wa chakula kwa kuzingatia makundi yote matano ya vyakula.