Milioni 300 ujenzi jengo la dharula Hospitali ya Wilaya
28 October 2021, 5:28 am
RUNGWE
katika kuendelea kuboresha huduma ya afya hapa nchini halmashauri ya wilaya ya Rungwe mkoani mbeya inatarajia kupokea fedha kutoka serikali kuu kiasi cha shilingi milioni 300 kwaajili ya ujenzi wa jengo la dhalura katika hosptali ya wilaya ya Rungwe [MAKANDANA]
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mh,MPOKIGWA MWANKUGA alipokuwa akizungumza na wanahabari ofisini kwa amesema ikiwa ni mkakati wa serikali ya awamu ya sita chini ya mweshimiwa rais samia suluhu hasani serikali imezamilia kuondoa changamoto wanazo kabiliana nazo wanachi pindi wanapo hitaji huduma za afya kwenye hospitali za wilaya nchini.
Aidha MWANKUGA amesema hamashauri ya rungwe imenufaika katika kumarisha miundombinu ya afya kwani katika kata ya kyimo serikali imetoa shilingi milioni 500 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya na ujenzi unaendelea na utakapo kamililika wananchi wa kata hiyo wanaondokana na adhaa ya kufuata huduma ya afya umbali mrefu.
kwa upande wa upatikanaji wa dawa kwenye dirisha la wazee mwenyekiti huyo amekili kuwa hapo nyuma alikuwa akipokea kero kutoka kwa wananchi kutokana na ukosefu wa dawa amesema kwaivi sasa changamoto ya ukosefu wa dawa imetatuliwa na amewataka watoe taarifa pindi watakapo kumbana na changamoto ya upatikanaji wa dawa katika hospitali hiyo.
sambamba na hayo amebainisha vituo vya afya viliyojenngwa ndani ya hamashauri ya Rungwe na vinavyoendelea kutoa huduma mpaka ivi sasa ikiwa ni pamoja na kituo cha afya Ikuti,Masukulu,Isongole na kituo cha afya mpuguso.