Milioni 500 kusaidia upatakanaji wa Maji Rungwe
27 October 2021, 5:22 am
RUNGWE.
Ofisi ya mamlaka ya maji Tukuyu Wilayani Rungwe mkoani Mbeya imeahidi kutatua changamoto ya maji kwa wananchi kupitia miradi inayoenda kutekelezwa ndani ya Wilaya.
Kupitia Meneja wa mamlaka ya maji Tukuyu Peter Amon amesema hayo akizungumza na Radio Chai kuwa serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 500 ambayo imetumika kununulia mabomba huku akisema mradi huo mpaka kukamilika utaghalimu shilingi bilioni nne.
Pia Amon amesema kuwa wameiomba Serikali fedha ili kukamilisha mradi kwa haraka na serikali imeahidi kutoa bilioni moja kwaajili ya kuendeleza mradi huo .
Hata hivyo amesema kumekuwa na ushiriki mdogo wa nguvu za wananchi katika kutekeleza mradi kikamilifu huku wakilazimika kumia fedha kwaajili ya kulipa vibarua.
Meneja wa mamlaka ya maji Tukuyu hakusita kuishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwajili ya kuboresha miundombinu ya maji Wilayani Rungwe.