Chai FM

Matumizi sahihi ya mswaki tiba ya kinywa

25 October 2021, 9:43 am

RUNGWE

Mratibu wa afya ya kinywa na meno Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya DOKT HOSEA MWAKYUSA ameelezea matumizi sahihi ya miswaki ambapo mswaki unatakiwa kutumika ndani ya miezi mitatu.

Akizungumza na kituo hiki amesema kuwa kinywa ni kitu muhumu katika kiungo cha binadamu na kinywa kimebebwa na vitu vikuu viwili ambapo  ni meno pamoja na ulimi na usafi wa kinywa hutegemeana na upigaji wa mswaki ambapo binadamu anaruhusiwa kuanza kutumia mswaki pale jino la kwanza linapoanza kuota.

Aidha amesema kuwa mswaki kwa kawida utakiwa utumike ndani ya miezi mitatu kwani mtu anapotumia mswaki zaidi ya miezi hiyo inapelekea mswaki kupoteza ubora na pale vimeleo vya mswaki vikiharibika kunauwezekano wa kukaribisha  maabukizi bakiteria aina ya faibasi na hupelekea magonjwa mbalimbali yanayoweza kuathiri mfumo wa kinywa ikiwa ni kutokwa na vidondo mdomoni na kutoboka kwa meno.

Hata hivyo ameelezea mahara salama pakuhifadhi mswaki pale mtu anapomaliza kupiga mswaki ili kizuia bakiteria ikiwa ni kutumia chombo maalumu cha kuhifadhia mswaki kile kinachopitisa mwanga kama vile glass yenye mfuniko na ametoa wito kwa jamii ambapo amesema kuwa kila mwananchi atumie mswaki kusafisha kinywa chake ndani ya miezi mitatu kwani knywa ni kiungo muhimu katika mwili wa binadamu.

Sambamba na hayo JAMES EDUWARD na HAPPY SAMWELI ambao ni wananchi nao wameeleza uelewa wao juu ya utumiaji wa mswaki  ikiwa ni kusaidia kuondoa harufu mbaya na kutunza meno na wameomba watalamu wa kinywa kutoa elimu zaidi kwa jamii juu ya matumizi ya mswaki katika kinywa.