Pangani FM

Taka, dhahabu iliyojificha yatajwa kuwa nyenzo kukabiliana na hewa ukaa

10/03/2026, 19:12

Baadhi ya vijana wakiwa katika kikao cha tathimini ya mafunzo ya udhibiti taka katika jengo la kituo cha redio Pangani FM

“Tunalishukuru shirika la UZIKWASA kwa kutupa mafunzo haya ya udhibiti wa taka, kwakuwa yametusaidia kutengeneza mkaa mbadala kupitia maganda ya ndizi kwasasa mazingira yetu ni safi”

Na Cosmas Clement

Baadhi ya vijana kutoka vijiji vya wilaya ya Pangani wamelipongeza shirika la Uzima Kwa Sanaa (UZIKWASA) kwa kuwawezesha katika kuchukua hatua ya udhibiti wa aina mbalimbali za taka katika maeneo yao.

Wakizungumza hii leo wakati wa zoezi la tathimini ya mafunzo ya udhibiti taka, vijana hao wamesema mafunzo hayo yamewawezesha kuzitumia taka kutengeneza bidhaa mbalimbali hivyo kuwaingizia kipato.

sauti za vijana wakielezea kunufaika na mafunzo ya udhibiti taka

Bi Gladnes Mgendi ambaye ni afisa vijana wilaya ya Pangani pamoja na kuwapongeza shirika hilo pia amewataka vijana kutokuwa na hofu katika kuziendea fursa zilizopo kupitia taka.

Sauti ya Gladnes Mgendi afisa vijana wilaya ya Pangani

Naye mwezeshaji kutoka shirika la UZIKWASA Bi Salvata Kalanga amewaasa vijana hao kuendelea kuwa mabalozi wazuri kwa kuhamaisha usafi wa mazingira katika maeneo yao.

Sauti ya Bi salvata kalanga

UZIKWASA kifupi cha Uzima Kwa Sanaa ni shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake wilayani Pangani limekuwa likitoa mafunzo ya mazingira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuchukua hatua dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi.