Pangani FM

Watoto Pangani waiangukia serikali ulinzi dhidi ya ukatili

18 June 2025, 1:41 pm

Mkuu wa wilaya ya Pangani Mhe. Gift Isaya Msuya

Tunaomba serikali na wadau mbalimbali kuwa na mikakati madhubuti ya pamoja itakayoimarisha ulinzi wa mtoto.

Na Hamisi Makungu

Watoto wilayani Pangani wameiomba serikali kushirikiana na wadau kuweka mikakati madhubuti ya pamoja katika kumlinda mtoto dhidi ya matukio ya kikatili ndani ya jamii.

Akizungumza kwa niaba ya watoto wa Pangani OMEGA GUSTAFU KAWICHE Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Kikokwe, ametoa rai kwa serikali na wadau mbalimbali kuwa na mikakati madhubuti ya pamoja itakayoimarisha ulinzi wa mtoto.

Sauti ya OMEGA GUSTAFU KAWICHE kwa niaba ya watoto wa Pangani

Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bi. Ester Gamba amegusia suala la malezi linavyochangia kuporomoka kwa maadili ndani ya jamii na kuchochea ukatili kwa watoto.

Sauti ya katibu tawala wa wilaya ya Pangani Esta Zulu Gama

Kwa upande wake Kaimu Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Pangani Bwana Linusi Richard amewataja watoto wa Wilaya ya Pangani kuwa wahanga wa ukatili wa kijinsia, ikiwemo kuozeshwa katika umri mdogo, kubakwa na kulawitiwa.

Sauti ya Kaimu Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Pangani Bwana Linusi Richard