Kitulo FM
Kitulo FM
20 January 2023, 7:00 pm
Ofisi ya Ardhi mkoa wa Njombe imeendesha zoezi la kukabidhi hati zipatazo Hamsini kwa wananchi wa kijiji cha Tandala wilayani Makete pamoja na kusikiliza changamoto za wananchi juu ya zoezi hilo leo Disemba 20 mwaka huu. Emmanuel Mkiwa kutoka ofisi…
19 January 2023, 8:03 am
Mahakama Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Januari 17, 2023 imemhukumu kifungo cha Miaka 30 jela Daudi David Mligo, mwenye umri wa miaka 26, mkazi wa Ludewa Mjini baada ya kukutwa na kosa la ubakaji. Mnamo Julai 16, 2022 majira ya saa tisa na dakika…
19 January 2023, 7:53 am
Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka akishirikiana na Jeshi la Polisi mkoani hapa, wamefika katika nyumba ambayo mfanyabiashara wa mbolea amekuwa akitumia kuchakachua bidhaa hiyo. Mtaka amesema katika nyumba hiyo isiyo na umeme, wamebaini mifuko ya makampuni mbalimbali ya mbolea, majenereta…
18 January 2023, 11:07 am
Ujenzi wa Kituo cha Afya Lupalilo awamu ya pili umefikia hatua nzuri baada ya kuwa katika hatua za mwisho wa ujenzi. Kituo hicho ujenzi wake ulianza kwa wananchi kujenga Jengo la wagonjwa wa nje na Serikali ikaunga mkono kwa…
18 January 2023, 10:39 am
Halmashauri ya mji wa Makambako imetakiwa kutoa elimu kuhusiana na usafi wa mazingira ili kuhakikisha maeneo yote yanafanyiwa usafi lengo likiwa ni kukabiliana na magonjwa ambukizi. Wakizungumza na Kituo hiki baadhi ya wananchi wa mtaa wa rajabu mahakamani uliopo…
18 January 2023, 10:04 am
WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe ameagiza kukamatwa kwa mmiliki wa Kampuni ya Candia Fresh pamoja na kuifunga kampuni hiyo, kwa kile alichoeleza kuwa inanunua parachichi ambazo hazijakomaa. Bashe amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikinunua parachichi hizo changa na kisha…
17 January 2023, 9:58 am
Wazazi kijiji cha Usagatikwa Kata ya Tandala na Ibaga Kata ya Mang’oto wamebainika kushawishi wanafunzi wafeli mitihani ya Darasa la Saba kwa maksudi. Kaimu Afisa Elimu Idara ya Msingi Wilaya ya Makete Mwalimu Bakari Msuya amesema kumekuwa na tabia…
17 January 2023, 9:31 am
Wananchi wa Kijiji cha Ihela Kata ya Tandala Wilayani Makete wameiomba Serikali kuangalia chanzo cha radi eneo la shule ili kuepusha hatari ya watoto kupigwa radi Wakizungumza na Kitulo Fm kwa nyakati tofauti wananchi hao wameeleza kuwa kumekuwa na…
17 January 2023, 9:02 am
MKAZI wa Matalawe mkoani Njombe, Furaha Lugenge (28) amefikishwa mahakamani kwa kosa la kumchoma moto mtoto wa mume wake sehemu za mapajani na kwenye makalio kwa kutumia moto wa mkaa kwa madai ya mtoto huyo kukojoa kitandani. Mbele ya…
17 January 2023, 8:57 am
Kijiji cha Usagatikwa wilayani Makete mkoani Njombe kipo kwenye hatari ya kukosa wasomi katika siku zijazo kutokana na wanafunzi wanaopangiwa kuanza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Lupalilo wengi wao kutohitimu kidato cha Nne Akitoa taarifa ya ripoti…
Kitulo Fm radio ni kituo cha kijamii kinachozalisha maudhui yenye hadhi ya kujenga jamii ya kitulo