Shinikizo la Damu changamoto zaidi kwa Wanaume Pangani.
12 November 2021, 5:02 pm
Magonjwa ya Sukari na Shinikizo la Damu la Juu yanaongoza kuwa na idadi kubwa ya Wagonjwa Wilayani Pangani Mkoani Tanga.
Takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha kuanzia Septemba 2020 hadi Septemba 2021 Jumla ya Wagonjwa wenye Shinikizo la Damu la Juu Wilayani Pangani walikuwa ni 2,436, huku Wagonjwa waliothibitishwa kuwa na Kisukari katika kipindi hicho walikuwa 584.
Aidha Wanaume Wilayani Pangani Wanatajwa kuongoza katika Magonjwa ya Shinikizo la Damu la Juu, huku Wanawake wakiongoza kwenye Magonjwa ya Kisukari.
Katika mazungumzo yake na Pangani FM Mratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza Wilaya ya Pangani Dkt. Rashid Mahmood Makoko amesema kuwa hatua za makusudi zinapaswa kuchukuliwa ili kukabiliana nayo.
“Kuna magonjwa mawili ambayo kwa kweli yanatishia Pangani, kuna Kisukari na kuna shinikio la juu la Damu (BP) kila siku kwenye Clinic na vito vyetu vya kutoa huduma tunaona namba inaongezeka hivyo tuchukue hatua za kukabiliana nayo haya”