Pangani FM

Michango hafifu ya chakula yatajwa kuathiri ujifunzaji wa watoto kitaaluma

8 October 2024, 3:53 pm

Walimu wawaangukia wazazi michango ya chakula shuleni

Na Hamis Makungu

Michango hafifu ya chakula kwa wanafunzi shuleni na mahudhurio madogo ya wazazi na walezi katika vikao shuleni, kunatajwa kuathiri ujufunzaji wa watoto kitaaluma.

Ameyasema hayo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Funguni iliyopo hapa Pangani Mjini Bi. Flora Mayaka katika risala aliyoisoma kwa niaba ya Shule mbele ya Mgeni Rasmi wakati wa Mahafali ya kuwaaga wahitimu 79 wa darasa la saba Mwaka huu.

Sauti ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Funguni Florah Mayaka

Akihutubia kwenye Mahafali hayo Mgeni Rasmi Kaimu Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bwana Mathias Pori aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo amewaasa wazazi kuona umuhimu wa upatikanaji wa chakula shuleni na ushiriki wao katika vikao kila vinapohitishwa

Sauti ya Kaimu Afisa Elimu (W) Pangani

Kwa miaka Minne mfululizo Shule ya Msingi Funguni imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma katika Matokeo ya ya mtihani wa darasa la saba.

Shule hiyo inajumla ya Wanafunzi 712, ambapo kwa darasa la Saba Mwaka huu Jumla ya wahitimu 79 wamefanikiwa kumaliza elimu ya msingi kati yao wavulana 30 na wasichana 49.