Pangani kuja na mkakati kabambe wa usafi
4 June 2024, 2:34 pm
Ni zaidi ya muongo mmoja umepita bila ya uwepo wa utatibu wa mdhabuni wa ukusanyaji taka hivyo kupelekea changamoto ya taka kuzaga katika mji wa Pangani kujaa.
Na Saa Zumo
Halmashauri ya wilaya ya Pangani imesema inaandaa mpango wa kudhibiti Taka kwa kutafuta mdhabuni atakaye zikusanya na kuzipeleka Dampo ili kuimarisha usafi wa mazingira katika halmashauri hiyo.
Hayo yameelezwa na Mdhibiti Taka na Usafi Wilayani Pangani Bwana Daniel Kijazi wakati akizungumza na kituo hiki na amekiri uwepo wa changamoto ya kuzagaa kwa taka kutokana na kukosekana miundombinu rafiki ya kuzikusanya.
Kwa upande wake Afisa Mazingira Wilaya humo Bwana Daud Mlahangwa amesema shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo husababisha uchakavu wa ardhi hivyo jamii inawajibu wa kuitunza kwa kupanda miti.
Naye Mkuu wa kitengo cha Maliasili Bwana Twahiru Mkongo akaisihi jamii wilayani PANGANI kutilia mkazo uhifadhi na utunzaji wa mazingira kwa maslahi ya afya zao na kuishi maeneo yaliyo salama.
Hayo yamejiri ikiwa Kesho Juni 5 ni maadhimisha ya kilele cha siku ya Mazingira duniani ambapo Halmashauri ya wilaya ya Pangani mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Pangani MUSSA KILAKALA na Kauli mbiu yake kwa mwaka huu 2024 ni ‘’urejeshwaji wa ardhi na ustahamilivu wa hali ya jangwa na ukame.’’