Pangani FM
Pangani FM
30 March 2026, 13:48

Kupitia ushirikiano wa kamati hizo wanafunzi wanafanya vizuri darasani kwakuwa wanapatiwa chakula shuleni.
Na Majabu Madiwa
Ushirikiano wa kamati za Mtakuwa, kamati ya shule na Kamati ya BMU katika kijiji cha Ushongo wilayani Pangani mkoani Tanga umetajwa kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika shule ya msingi ushongo.
Hayo yamebainishwa katika zoezi la ufuatiliaji na tathmini linalofanywa na shirika la Uzikwasa kwa kamati hizo.
Katika kikao kilichokutanisha kamati hizo Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bw. Abdallah Makuka ameeleza namna ushirikiano baina yao ulivyowezesha kambi ya masomo kwa wanafunzi wa darasa la saba mwaka 2025.
Stambuli Ramadhan ni mwalimu wa shule ya msingi Ushongo hapa anaeleza namna kambi hiyo ya masomo ulivyoongeza ufaulu kutoka asilimia 149 kwa mwaka 2024 hadi asilimia 170 kwa mwaka 2025.
Aidha Mwl Stambuli ameelezea namna shule hiyo inavyonufaika na jiko banifu katika shughuli za upishi wa chakula cha wanafunzi,jiko lililowezeshwa na shirika la UZIKWASA.
Miongoni mwa mikakati ya kamati hizo ni kuhakikisha upatikanaji wa chumba cha kujisitiri wanafunzi wa kike, kuwezesha uji kwa wanafunzi wote na wanafunzi wa madarasa ya mitihani yaani la nne na la saba waweze kupata chakula shuleni