Pangani FM

Ireland wafurahishwa, UZIKWASA kuvifikia vikundi vya kijamii Handeni

19 March 2026, 23:39

Kaimu mkuu wa wilaya ya Handeni ambay ni Afisa Tarafa ya Kwamsisi Bwana Lugaila Nkwabi akizungumza wakati wa ziara hiyo

“Tunaomba maafisa maendeleo ya jamii kata zote kutoa ushirikiano na wilaya tunaomba muwe na kipaumbele kusimamia mradi huu” Bi Oliver

Na Cosmas Clement

Wawakilishi kutoka Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania wamesema wameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa kuongeza uwezo kwa vikundi vya kijamii katika halmashuri ya wilaya ya Handeni  unaoendeshwa na  shirika la UZIKWASA lenye makao yake wilayani Pangani.

Wawakilishi hao wameyasema hayo hii leo wakati wa ziara ya kupitia na kutathimini maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo wenye lengo la kuwezesha  vikundi hivyo vya  kijamii wilayani Handeni kufikia usawa wa kijinsia na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo meneja wa mradi  Bi Oliver Kinabo kutoka ubalozi wa Ireland, amelipongeza shirika la UZIKWASA kwa kuwezesha vikundi mbalimbali vya wanawake na vijana ambavyo vimekuwa ni chachu ya mabadiliko katika jamii yao.

sauti ya Oliver Kinabo kutoka ubalozi wa Ireland

Akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Handeni ambaye ndiyo alikuwa mgeni rasmi,  kaimu mkuu wa wiaya hiyo Bwana  Lugaila Nkwabi amewataka watendaji na maafisa maendeleo  ya kata zinazotekelezwa mradi huo, kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi huo ili kufikia mafanikio yanayolengwa.

sauti ya Bwana  Lugaila Nkwabi
Baadhi ya maafisa mandeleo kata zinazonufaika na mradi huo, wakiwa pamoja na mgeni rasmi na wakilishi wa Ireland na UZIKWASA

Kwa upande wake mwezeshaji kutoka shirika la UZIKWASA  bwana Erick Malya amesema kupitia mradi huo vikundi mbalimbali vilivyopo kata tano vimejengewa uwezo ili kuwezesha wanawake na vijana kiuchumi ili kukabiliana na matukio ya ukatili na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Sauti ya Erick Malya

Katika ziara hiyo Shirika la UZIKWASA na wawakilishi kutoka Ubalozi wa Ireland wamekutana na wakuu wa idara na wakuu wa vitengo mbalimbali pamoja na mwakili wa mguu wa wilaya ya handeni ili kutathimini maendele ya mradi huo.

UZIKWASA ni shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kuwajengea uwezo wnajamii katika kuchukua hatua za usawa wa kijinsi na mabadiliko ya tabia nchi.