Pangani FM

Mbunge wa Jimbo la Pangani akabidhi photocopy machine ya milion 8

09/03/2026, 13:58

Katibu wa mbunge wa jimbo la Pangani bwana Salmin Mmari mwenye t-shirt ya njano akikabidhi mashine ya photocopy kwa shule ya uongozi wa shule ya sekondari Muhembo. Mwl. Mmari aliongozana na wawakilishi wengine wa ofisi ya Mbunge akiwemo Bi Aisha Msofe

Na Cosmas Clement

Mbunge wa jimbo la Pangani na waziri wa maji Mhe. Juma Hamidu Aweso hii leo amekabidhi mashine moja ya kudurufu nakala (photocopy machine) yenye thamani ya shilingi milioni nane kwa shule ya sekondari Muhembo iliyopo kijiji cha Pangani Mashariki wilayani Pangani.

Akikabidhi mashine hiyo kwa niaba ya mbunge huyo, Katibu wa mbunge wa jimbo la Pangani Mwl. Salmini Mmari kutolewa kwa mashine hiyo ni muendelezo wa jitihada za kuboresha kiwango cha ufaulu katika wilaya ya Pangani.

Sauti ya katibu wa mbunge Juma Aweso

Mkuu wa shule ya sekondari Muhembo Mwl. Ernesta Mwakamela amesema kupatikana kwa mashine hiyo itasaidia kupunguza changamoto za upatikanaji wa huduma za uchapishaji wa mitihani.

Sauti ya Mwl. Mwakamela
Picha wanafunzi wa shule ya Sekondari Muhembo wakishuhudia mashine ya photocopy ikifunguliwa. Mashine hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Pangani

Bwana Peter Mabuga mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari ya Muhembo amemshukuru Mbunge huyo kwa kutoa mashine hiyo akiwaasa wanafunzi na walimu kuitunza mashine hiyo iweze kudumu kwa muda mrefu.

Sauti ya Mabuga

Ofisi ya mbunge wa jimbo la Pangani imekuwa ikitoa misaada mbalimbali inayolenga kutatua changamoto za kielimu ili kuinua sekta ya elimu wilayani humo.