Pangani FM

Watu wawili wanusurika mnazi ukivunja nyumba usiku

26/02/2026, 18:51

Nyumba ikiwa imeangukiwa na mnazi kufuatia mvua kubwa iliyonyesha jumatano usiku katika kijiji cha Pangani Magharibi.

‘Niliposhituka nilijiona kama nakandamizwa na vitu vizito, lakini namshukuru Mungu nipo hai. Naomba msaada wa kujenga upya nyumba mimi uwezo wangu mdogo nyumb yote imeanguka” Bahati Omary

Na Cosmas Clement

Watu wawili wa familia moja wanaoishi katika mtaa wa majengo kijiji cha Pangani Magharibi Mkoani Tanga, wamenusurika,  kufuatia mnazi kuangukia na kuharibu nyumba walimokuwa wamelala usiku wa kuamkia alhamisi.

Akithibitisha tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji cha Pangani Magharibi wilayani Pangani Mkoani Tanga, Bwana Salumu Kanyama amesema ajali hiyo imetokea usiku kutokana na mvua kubwa iliyoambata na radi wakati mama huyo na mtoto wake wakiwa wamelala.

Sauti ya mwenyekiti wa Pangani magharibi bwana Salum Kanyama

Amesema kutokana na ajali hiyo, kijiji hicho kimeanza kuchukua hatua kumsaidia mama huyo baada ya kufanyika kwa tathimini ya madhara yaliyotokea .

Sauti ya mwenyekiti wa Pangani magharibi bwana Salum Kanyama

Kwa upande wake mama aliyekutwa na ajali hiyo anayefahamika kwa jina la Bahati Omary Bakari ameiomba  serikali na wanajamii kumsaidia katika kipindi hiki kwani kwa sasa hana sehemu salama ya kulala.

Sauti ya Bahati Omary muhanga wa ajali hiyo