Pangani FM
Pangani FM
25 February 2026, 3:08 pm

Na Saa Zumo
Maafisa elimu nchini wametakiwa kujadili muongozo wa adhabu za viboko mashuleni ili kuepuka vipigo vilivyopitiliza kwa wanafunzi.
Hayo yameelezwa Februari 24 2026 na Waziri wa maendeleo ya jamii, wanawake, watoto na makundi maalumu Muheshimiwa Dorothy Gwajima wakati akizungumza na baadhi ya wakuu wa Idara wilayani Pangani katika ofisi za mkuu wa wilaya hiyo.
Katika kikao hicho Waziri Gwajima amewataka walimu kutoa adhabu kulingana na miongozo iliyopo nchini.
Hata hivyo Waziri DOROTHY GWAJIMA amewataka maafisa utamaduni nchini kupaza sauti na kukemea maadili mabovu kwa kushirikiana na sekta zilizopo katika maeneo yao.
Uwepo wa changamoto ya mmomonyoko wa maadili kwa vijana na watoto nchini unatajwa kuchangiwa na baadhi ya watu wakubwa huku wakiagizwa kupaza sauti ya kuhenzi maadili mema kwa jamii.
Hayo yamejiri hii katika ziara ya siku moja wilayani Pangani iliyofanywa naWaziri wa maendeleo ya jamii, wanawake, watoto na makundi maalumy Muheshimiwa Dorothy Gwajima ambapo amepata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wakuu wa Idara katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Pangani, na kushiriki zoezi la kupanda miti Kijiji cha Jaira kata ya Madanga huku akipata nafasi ya kutembelea shirika la Uzikwasa ili kuona namna linavyofanyakazi wilayani humo