Pangani FM
Pangani FM
18 February 2026, 7:29 pm

“Mafunzo haya yamenihuisha maarifa ya kiuongozi, kujitathimini na uwezo wa kuwasikiliza wananchi na nimejifunza kwamba unapokuwa kiongozi unapaswa kuwa na mguso hususani katika kusikiliza mwananchi”
Na Cosmas Clement
Wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri ya wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, wamelishukuru shirika la UZIKWASA kwa mafunzo ya uongozi wa Mguso waliowapa kwani imewasaidia kubadilisha baadhi ya mitazamo katika nafasi zao za uongozi.
Hayo wameyazungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo ya uongozi wa mguso yaliyotolewa kwa siku mbili katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo wakisema mafunzo hayo yamewasaidia kujiongezea maarifa ya uongozi na uwezo wa kusikiliza wananchi.
Naye mkuu wa idara ya utawala na usimamizi wa rasilimali watu Bi Gladness Mwano ambaye ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo, amesema siku mbili za mafunzo wa wakuu hao wa idara na vitengo itasaidia kubora mahusiano na utendaji kazi.
Kwa upande wake Mariamu Ally mwezeshaji kutoka shirika la UZIKWASA amewaomba washiriki hao wa mafunzo kuyaambukiza mafunzo hayo kwa wafanyakazi wengi ili kuwa na timu yenye mahusiano mazuri kazini.