Pangani FM

Hivi ndivyo uchumi wa wana-Pangani utakavyokuwa

16 February 2026, 11:27 pm

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta Mwigulu Nchemba akagua ujenzi wa daraja la mto Pangani lenye urefu wa mita 525.

“Ujenzi wa barabara hii na daraja la Mto Pangani imeweka alama isiyofutika katika wilaya ya Pangani”

Na Cosmas Clement

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta Mwigulu Nchemba ameiagiza wizara ya ujenzi kuhakikisha vipande vya barabara vinavyoendelea kujengwa vinakamilika kwa wakati katika mradi wa barabara ya Tanga, Pangani Bagamoyo ili kuvutia maendeleo ya wilaya ya Pangani.

Dkt. Nchemba ametoa agizo hilo katika ghafla ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa daraja la Mto Pangani lenye urefu wa mita 525, akisema mradi huo utasaidia kuinua uchumi wa wananchi wa wiaya ya Pangani.

Sauti ya waziri mkuu wa JMT Mwigulu Nchemba

Kwa upande wake Naibu waziri wa ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema mradi huo wa barabara utawezesha kuweka taa zaidi ya 400 katika njia zote za mji wa Pangani.

Sauti ya Kasekenya Naibu waziri Ujenzi
Picha za juu zikionesha daraja la Mto Pangani linaloendelea kujengwa

Awali akizungumza katika ghafla hiyo ya ukaguzi wa daraja la Mto Pangani Mbunge wa jimbo hilo na Waziri wa Maji, Mhe Juma Hamidu Aweso ameiomba serikali kuweka bandari ya mifugo katika wilaya ya Pangani ili kurahisisha biasha ya mifugo pamoja na kuwawezesha wananchi kuendesha kilimo cha umwagiliaji kupitia mto pangani.

Sauti ya Juma Aweso mbunge wa jimbo la Pangani