Pangani FM

Jamii, serikali kushirikiana kumlinda mtoto

11 October 2024, 4:09 pm

Picha ya Viongozi walioshiriki siku ya Mwalimu Conference

“Wito wangu kwa wadau ni kutunga sera ambazo zitakuwa na manufaa kwa kizazi cha sasa na baadae” Mwezeshaji kutoka Shirika la UZIKWASA Bwana Nickson Lutenda

Na Kokutona Banyikila

Jamii imeshauriwa kuendelea kushirikiana na serikali kutengeneza mifumo iliyo salama kwa ajili ya ulinzi wa mtoto na kumjengea uwezo utakaosaidia kupata wataalam wa baadae ambao watalisaidia taifa letu kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

Ushauri huo umetolewa na muwezeshaji kutoka shirika la UZIKWASA Bwana Nickson Lutenda aliposhiriki mdahalo wa ufungunguzi wa kampeni ya Mtoto wa leo Samia wa kesho iliyofanyika katika wilaya ya Muheza mkoani Tanga

Sauti ya Bwana Nickson Lutenda

Pia ametoa wito kwa wadau kutengeneza sera ambazo zitalenga kusaidia kizazi cha sasa na baadae na kuacha alama katika taifa hili

Sauti ya Bwana Nickson Lutenda