Pangani FM

Wakulima washindwa kulima, maji ya mto kuvamia mashamba yao

8 September 2024, 4:08 pm

Mto Msangazi unaopita katikati ya mashamba ya wakulima kijiji cha Mbulizaga umevunja kingo zake kutokana na shughuli za binadamu.

Baadhi ya wakulima wamelamizika kuazima mashamba ili kuendesha shughuli zao kutokana na mashamba yao kuvamiwa na maji ya mto Msangazi.

Wakulima katika kijiji cha Mbulizaga wilayani Pangani wameiomba serikali kuwasaidia kutengeneza ukingo wa mto Msangazi uliopo kijijini hapo ambao ulivunja kingo zake na kupelekea mafuriko katika mashamba yao.

Wakizungumza na Pangani FM wakulima hao wamesema kutokana na mafuriko hayo imewalazimu kuacha kulima katika mashamba yao hali inayotishia ugumu wa upatikanaji wa chakula.

Sauti ya wakulima Mbulizaga

Aidha wamesema chanzo cha kuvunjika kwa kingo za mto huo ni shughuli za binadamu ikiwemo unyweshaji mifugo katika bonde la mto huo.