Pangani FM

TCRA kuwabaini wezi wa ‘tuma kwa namba hii’

29 August 2024, 3:17 pm

Mhandisi Francis Mihayo meneja TCRA Kanda ya Kaskazini akifanya mahojiano na kituo cha Pangani FM

Uhalifu wa kimtandao umekuwa ukichukua sura mpya siku hadi siku ingawa serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukabiliana nao.

Na Cosmas Clement

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  amewaasa wanajamii kuwa makini na  matumizi ya mitandao ili kulinda usalama wa mali zao na faragha.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Kaskazini Mhandisi Fransic Mihayo wakati akizungumza na kituo hiki cha redio.

Mhandisi Mihayo amesema ipo athari kubwa endapo wanajamii hawatakuwa makini katika matumizi salama ya mitandao.

Mhandisi Francis Mihayo meneja TCRA Kanda ya Kaskazini

Amesema mtumiaji wa mitandao anapaswa kulinda taarifa zake muhimu ili zisiweze kuathiriwa na wenye nia mbaya.

Mhandisi Francis Mihayo meneja TCRA Kanda ya Kaskazini

Amesema endapo mtu yeyote akikutana na ujumbe unaosema tuma kwenda kwenye namba hii, atoe taarifa kwa TCRA kupitia namba ya ujumbe mfupi 15040.

Mhandisi Francis Mihayo meneja TCRA Kanda ya Kaskazini