Pangani FM

Kura 17 za ndio zampitisha makamu mwenyekiti Pangani DC

31 July 2024, 4:33 pm

Makamu mwenyekiti wa halmashauri Mhe, Zainabu Mvaa akishukuru madiwani waliompigia kura za ndio katika kikao cha baraza la madiwani.

Ni kawaida kila mwaka wa fedha baraza la madiwani hupiga kura kumchagua makamu mwenyekiti wa halmashauri anayeongoza kwa mwaka mmoja.

Na Cosmas Clement

Baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Pangani July 31 2024 limempitisha kwa mara nyingine Mheshimiwa Zainabu Mvaa diwani wa viti maalumu tarafa ya Mwera kuwa makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani

Matokeo ya uchaguzi huo yametangazwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mheshimiwa Akida Bahorera  katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo.

Sauti ya mwenyekiti wa Pangani DC

Mhe, Bahorera amesema uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa halmashauri na wenyeviti wa kamati kwa kawaida hufanyika mwaka wa fedha unapofika mwisho.

Sauti ya mwenyekiti wa Pangani DC Mhe, Akida BAHORERA

Kwa upande wake Bi Zainabu amewashukuru madiwani kwa kuendelea kumuamini kutumikia nafasi hiyo na kuahidi kutekeleza wajibu wake ili kuiletea maendeleo halmashauri ya wilaya ya Pangani.

Sauti ya makamu mwenyekiti bi Zainabu Mvaa

Bi Zainabu ambaye ni diwani wa viti maalumu wa tarafa ya Mwera amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri kwa mara ya tatu mfululizo.