Pangani FM

Wajawazito Pangani waaswa kuwahi kliniki

25 July 2024, 2:50 pm

Baadhi ya wanawake wa kijiji cha Pangani Mashariki wakimsikiliza afisa lishe wilaya ya Pangani.

Mara nyingi wajawazito huchelewa kuanza kliniki ya ujauzito hali inayotajwa kuleta ugumu katika kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza.

Na Cosmas Clement

Wito umetolewa kwa mama wajawazito wilayani Pangani kuanza kliniki mapema ili kupunguza changamoto za kiafya zinazoweza kujitokeza.

Akizungumza katika siku ya Afya na Lishe afisa lishe kwa kijiji cha Pangani Mashariki wilayani humu,Bwana Daudi Mwakabanje ambaye ni Afisa lishe wilaya ya Pangani, amesema kuanza kliniki kwa wakati kutamuwezesha mjamzito kukabiliana na changamoto za kipindi cha ujauzito.

Sauti ya bwana Daudi Mwakabanje afisa lishe wilaya ya Pangani

Bwana Mwakabanje amewahamasisha wakinamama kuzingatia kanuni sahihi za unyonyeshaji kwa watoto ili kupunguza udumavu.

Sauti ya bwana Daudi Mwakabanje afisa lishe wilaya ya Pangani

Bi Fatuma Chee diwani wa viti maalumu wa Pangani Mjini amewasisitiza wakinamama kuzingatia elimu waliyoipata na kuwaelimisha wengine.

Sauti ya diwani wa viti maalumu Pangani Mjini Mhe Fatuma Chee