Pangani FM

DC Pangani, ni marufuku masomo ya usiku

25 June 2024, 9:59 am

Mkuu wa wilaya ya Pangani Bwana Mussa Ramadhan Kilakala aliyesimama katikati.

Uchunguzi wabaini watoto 26 wa shule moja kulatiwa.

Na Hamisi Makungu

Mkuu wa Wilaya ya Pangani Musa Ramadhan Kilakala amepiga Marufu Wanafunzi kurudi Shuleni usiku, huku akitaka  muda wa masomo uzingatiwe.

DC Kilakala ametoa Marufuku hiyo baada ya hivi karibuni kuzungumzia uchunguzi uliobaoni moja ya Shule Wilayani Pangani Watoto zaidi ya 26 wamelawitiwa.

Sauti ya DC Mussa Kilakala

Sambamba na hilo DC KIlakala amepiga Marufuku biashara ya Pombe kufanyika majumbani, huku akimuagiza Afisa Biashara kuhakikisha maeneo yote yanayofanya biashara kinyume na utaratibu kufungiwa.

Sauti ya DC Mussa Kilakala