Pangani FM

RC Tanga: Hakikisheni mpaka June 28 hoja 19 zimejibiwa

22 June 2024, 10:37 am

Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Buriani katikati kushoto kwake ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Pangani Mhe. Akida Bahorera na kulia ni RAS wa mkoa wa Tanga katika kikao cha baraza la madiwani.

Pamoja na kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 halmashauri ya wilaya ya Pangani imekuwa na hoja nyingi ambazo hazijajibiwa ikiwemo kumi na tisa za kamati ya kudumu ya Bunge.

Na Cosmas Clement

Halmashauri ya wilaya ya Pangani imepewa siku sita kuanzia Jumamosi ya leo kujibu hoja kumi na tisa za kamati ya kudumu ya Bunge zilizotolewa katika ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Buriani katika kikao cha Baraza la madiwani cha kujadili na kupitia hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali katika kipindi cha mwaka fedha uliopita.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga

Awali akiwasilisha taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali, Bwana Gudlucky Minja amesema halmashauri ya Wilaya ya Pangani ina hoja zipatazo thelathini na tisa ambazo hazijajibiwa.

Sauti ya mkaguzi wa hesabu za serikali Gudlucky Minja

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Pangani Bwana Edward Charles Fussi amesema halmashauri imepokea maelekezo hayo na inaendelea kufanyia kazi kujibu hoja hizo.

Sauti ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Pangani Edward Fussi

Pamoja na hoja hizo kutojibiwa, halmashauri ya wilaya ya Pangani katika kipindi cha mwaka fedha 2022/23 imefanikiwa kupata hati safi ambayo inakuwa ni mwaka sita mfululizo kupata hati hiyo.