Pangani FM

Talaka sababu ya ulawiti kwa watoto Pangani

10 June 2024, 9:51 pm

Baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi wakiwa katika kikao cha kutathimini na kuibua mikakati ya kukabiliana na matukio ya ukatili wilaya ya Pangani.

Matukio ya ukatili ikiwemo ulawiti, inatajwa kuendelea kutokea ingawa jitihada za wadau zikifanyika dhidi ya matukio hayo huku utelekezaji familia, ushirikina na wazazi kutengana zikitajwa kuwa ni sababu.

Na Cosmas Clement

Shirika la Uzima kwa Sanaa (UZIKWASA) lililopo wilayani Pangani mkoani Tanga limewakutanisha wajumbe wa kikosi kazi wilayani humo ili kujadili, kutathmini na kuibua mikakati ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Wakizungumza katika kikao hicho wajumbe hao wameelezea kuguswa na matukio ya ukatili, ubakaji na ulawiti yanayotokea wilayani humo yanayopelekea kuharibu ndoto na maisha ya  watoto.

Miongoni mwa sababu zilizotajwa na wajumbe hao ni pamoja na wazazi kutengana, utelekezaji wa watoto, imani za kishirikina pamoja na tabia ya baadhi ya  wazazi kulala pamoja na watoto wao.

Sauti ya wajumbe wa kikosi kazi

Kwa upande wake mwezeshaji kutoka shirika la UZIKWASA bwana Nickson Lutenda amewasihi wajumbe hao kuangalia namna bora ya  kushughulikia matukio hayo bila ya kuathiriwa na dhana binafsi.

Sauti ya mwezeshaji katika mafunzo hayo Nickson Lutenda

Mwezeshaji mwingine kutoka UZIKWASA Bi Salvata Kalanga amewataka wajumbe hao kutengeneza mkakati wa pamoja kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia.

Sauti ya Mwezeshaji Salvata Kalanga

Kikao hicho ni muendelezo wa shughuli za shirika la UZIKWASA katika kuwawezesha wadau mbalimbali kuboresha utendaji katika kukabilina na vitendo vya ukatili, ambapo miongoni mwa wanaounda kikosi kazi hicho ni wawakilishi kutoka idara mbalimbali za halmashauri, Mkuu wa Wilaya na jeshi la polisi.