Pangani kuanza mradi, nishati safi ya kupikia
10 June 2024, 9:28 pm
Mradi wa nishati safi ya kupikia utawawezesha wananchi wa Pangani kunufaika na biashara ya hewa ya ukaa.
Na Majabu Madiwa
Shirika la kuhifadhi misitu ya asili nchini Tanzania (TFCG) limeanza kutambulisha mradi wa nishati safi katika halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga.
Hayo yamesemwa na afisa mazingira Wilaya ya Pangani BW DAUDI MLAHAGWA ambapo amevitaja vijiji vitakavyonufaika ni Mseko Mtango na Kwakibuyu.
Aidha BW MLAHAGWA amesema ujio wa wadau mbalimbali wa mazingira Wilayani Pangani utaendelea kuchagiza umuhimu wa utunzaji wa mazingira.
Hatua hii ni jitihada za halmashauri katika kutafuta wadau wa nishati safi ambapo tayari mradi huo umekwisha tambulishwa katika ngazi ya Wilaya na hatua iyiyopo kwa sasa ni utambulisho wa mradi katika ngazi ya vijiji huku wananchi wakitarajiwa kunufaika kupitia bishara ya hewa ukaa.