Ufaulu Darasa la Saba 2020 washuka Wilayani Pangani.
2 December 2020, 4:43 pm
Ufaulu kwa wanafunzi waliohitimu Darasa la Saba Wilayani Pangani kwa mwaka 2020 umetajwa kushuka kwa Asilimia 6.74% ukilinganishwa na Mwaka jana.
Akizungumza na Pangani fm Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani amesema ufauu huo umeshuka ukilinganisha na mwaka jana ambo ulikuwa ni asilimia 82.1 huku akisema kuwa Janga la COVID-19 liliathiri kwa namna moja ama nyingine.
“Kwa tathimini ya awali tumeona katika kipindi cha mwezi Machi hadi mwezi June kile kipindi cha COVID-19 watoto walikuwepo nyumbani,pamoja na jitihada tulizofanya kwa kushirikiana na radio kufanya vipindi lakini bado pengo limeonekana kuwa ni kubwa wanafunzi walishindwa kutumia kipindi hiko kuendelea na masomo”
Amesema DED Isaya Mbenje.
Aidha Bwana Mbenje amesema wanafunzi 18 ambao ni sawa na asilimia 1.8 ndio ambao hawakufanya mtihani,kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro sugu.
Watoto ambao hawakufanya mtihani tumegundua kwamba tatizo kubwa ilikuwa ni utoro,na wengine walipata mimba katika kipindi cha nyuma walishindwa kufanya mitihani,ila yote kwa yote utoro ndio ilikuwa sababu kubwa,.
Amesema DED Isaya Mbenje
Wanafunzi 1012 kati ya 1362 ambao ni sawa na asilimia 75.36 wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza January mwakani.