Wasafirishaji wa Mchanga watakiwa kuchukua tahadhari za mazingira.
17 March 2021, 7:02 pm
Wachimbaji wa vifusi vya Mchanga na Mawe Wilayani Pangani Mkoani Tanga wametakiwa kuhakikisha kuwa shughuli za uchimbaji zinazingatia usalama wa mazingira na afya za binadamu ili kuepusha madhara yanayoweza kuepukika.
Wito huo umetolewa na Kaimu Afisa Mazingira Wilaya ya Pangani Bwana Twahiru Mkongo, ambapo amesema kuwa ni vyema wachimbaji wa vifusi kuzingatia usalama katka usafirishaji wa vifusi ili vumbi lisiathiri watu wengine sambamba na kurejesha katika hali yake maeneo wanayoyatumia.
Hawa wachimbaji wa vifusi tahadhari wanazopaswa kuzichukua nikuhakikisha wanapomaliza kuchimba kujitahidi kulirudisha eneo kama lilivyokuwa na wanaposafirisha material wasimwage vumbi wamwage maji ilikuwalinda wananchi
Amesema Bwana Twahiru Mkongo
Aidha Bwana Mkongo amesema kuwa endapo mashimo yanayochimbwa yakiachwa kiholela yanaweza kuleta athari katika jamii.
Uchimbaji wa madini ya mawe na vifusi licha ya kutumiwa katika ujenzi ikiwemo wa makazi pia shughuli hiyo imekuwa ikitoa ajira kwa wilaya ya pangani huku wataalamu wa maingira wakieleza kuwa shughuli hiyo haijaleta athari kubwa kwa mazingira na binadamu
Aesema Bwana Mkongo
Ukichimba na kuondoka unaweza kuacha mashimo hatarishi kama shimo ni refu kwa mana hiyo ilikuepuka maafa tujitahidi kuyarudishia ili uoto wa asili uweze kurejea katika hali yake
Amesema Bwana Mkongo