Pangani FM

Changamoto za kijamii zatajwa kuchangia tatizo la afya ya akili kwa watumishi

11 October 2024, 3:03 pm

Picha kwa hisani ya mitandao ya kijamii

“Changamoto ya afya ya akili inaweza kumkuta mtu yeyote bila kujali cheo au nafasi yake” Mtaalam wa afya ya akili kutoka Hospitali ya Wilaya ya Pangani Vicent Tarimo

Na Hamis Makungu

Changamoto za kijamii ikiwemo hali ya kimaisha zimetajwa kuchangia tatizo la afya ya akili kwa watumishi katika maeneo ya kazi.

Hayo yanajiri wakati leo Oktoba 10 Tanzania ikiungana na Mataifa mengine Dunia ikiadhimisha Siku ya Afya ya akili, ambayo Mwaka huu Maadhimisho hayo yanabebwa na kauli mbiu inasemayo “Ni wakati wa kuipa kipaumbele Afya ya akili Mahali pa kazi”.

Akizungumza na Pangani hii leo Mtaalam wa afya ya akili kutoka Hospitali ya Wilaya ya Pangani Vicent Tarimo amewataka watumishi katika maeneo yao ya kazi kutambua kwamba changamoto ya afya ya akili inaweza kumkuta mtu yeyote bila kujali cheo au nafasi yake.

Sauti ya Vicent Tarimo

Amesema takwimu za Shirika la Afya WHO zinakadiria kuwa 60 ya wafanyakazi duniani wanakabiliwa na msongo wa mawazo, na kwamba hadi kufikia mwaka 2050 magonjwa ya akili yataongoza kwa vifo na ongezeko la idadi ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu ya akili hospitalini.

Sauti ya Vicent Tarimo

Shirika la Afya linasisitiza kwamba Mazingira salama na yenye afya ya kufanya kazi yanaweza kuwa sababu ya kinga kwa afya ya akili.