Shirika la TFCG kutambulisha mradi wa nishati safi wilayani Pangani
16 August 2024, 1:57 pm
Kutoka kushoto mwenye shati la kijivu mikono mirefu ni afisa mazingira halmashauri ya wilaya ya Pangani akiwa katika kituo cha redio Pangani FM.
Serikali imekuwa ikiendelea kutekeleza mkakati wa matumizi ya nishati safi kwa kushirikiana na mashirika na wadau mbalimbali wa mazingira ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Na Saah Zumo
Shirika la kuhifadhi misitu ya asili nchini Tanzania (TFCG) limeanza kutambulisha mradi wa nishati safi katika halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga.
Hatua hii ni jitihada za halmashauri katika kutafuta wadau wa nishati safi ambapo tayari mradi huo umekwisha tambulishwa katika ngazi ya Wilaya na hatua iyiyopo kwa sasa ni utambulisho wa mradi katika ngazi ya vijiji huku wananchi wakitarajiwa kunufaika kupitia bishara ya hewa ukaa.
Hayo yamesema na afisa mazingira Wilaya ya Pangani BW DAUDI MLAHAGWA ambapo amevitaja vijiji vitakavyonufaika ni Mseko Mtango na Kwakibuyu.
Aidha BW MLAHAGWA amesema ujio wa wadau mbalimbali wa mazingira Wilayani Pangani utaendelea kuchagiza umuhimu wa utunzaji wa mazingira.