Wajawazito Pangani waaswa kuwahi kliniki
25 July 2024, 2:50 pm
Mara nyingi wajawazito huchelewa kuanza kliniki ya ujauzito hali inayotajwa kuleta ugumu katika kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza.
Na Cosmas Clement
Wito umetolewa kwa mama wajawazito wilayani Pangani kuanza kliniki mapema ili kupunguza changamoto za kiafya zinazoweza kujitokeza.
Akizungumza katika siku ya Afya na Lishe afisa lishe kwa kijiji cha Pangani Mashariki wilayani humu,Bwana Daudi Mwakabanje ambaye ni Afisa lishe wilaya ya Pangani, amesema kuanza kliniki kwa wakati kutamuwezesha mjamzito kukabiliana na changamoto za kipindi cha ujauzito.
Bwana Mwakabanje amewahamasisha wakinamama kuzingatia kanuni sahihi za unyonyeshaji kwa watoto ili kupunguza udumavu.
Bi Fatuma Chee diwani wa viti maalumu wa Pangani Mjini amewasisitiza wakinamama kuzingatia elimu waliyoipata na kuwaelimisha wengine.