Pangani FM

Kilio, fidia kwa baadhi ya wananchi waliopisha barabara

27 June 2024, 10:27 pm

Picha ya barabara ya Lami. Picha kutoka Mtandaoni

Ujenzi wa barabara ya lami kutoka Tanga yenye urefu wa Km 50 unagharimu shilingi za kitanzania bilioni 66.853

Na Hamisi Makungu

Kilio cha Madai ya fidia kwa Wananchi waliochukuliwa maeneo yao kupisha Mradi wa Barabara Tanga-Pangani-Saadani-Bagamoyo bado Donda ndugu.

Kilio hicho kimewasilishwa na Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tanga Mhandisi Dastan Singano.

Madiwani hao wamesema kilio kwenye suala hilo la Malipo ya fidia kimeacha maumivu kwa wananchi ambao kutokana na tathmini ya awali kuonesha watalipwa fidia zao, lakini hadi sasa bado hawajalipwa kwa madai kwamba walikuwa ndani ya eneo la barabara.

Sauti ya madiwani

Akijibia Kilio hicho Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tanga Mhandisi Dastan Singano amesema taarifa alizo nazo hadi sasa ni kwamba watu wote waliostahili kulipwa fidia zao tayari wameshalipwa.

Sauti ya meneja wa Tanroads mkoa wa Tanga

Ujenzi wa barabara hiyo uliotiwa saini mwezi julai mwaka 2019 kwa sasa upo katika hatua ya utekelezaji baada ya baadhi ya wananchi waliohakikiwa kulipwa fidia zao.