Pangani FM

Wapeni watoto haki zao

22 June 2024, 9:56 am

Picha ikionyesha haki za watoto. Picha kutoka mtandaoni.

Kutokana na matukio ya ukatili kuongeza wazazi na walezi wengi wamekuwa wakiwazuia watoto wao kucheza ama kuwapa muda mchache wa kucheza.

Na mwandishi wetu.

Wazazi na walezi wilayani panagani wametakiwa kuwapa uhuru watoto wao ikiwemo uhuru wa kucheza na kusikilizwa.

Wito huo umetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii Pangani Bwana KIRIGITI ENOCK, ambapo amesema wazazi wengi wameshindwa kuwapatia watoto wao uhuru wa kucheza na kusikilizwa wakidhania kwamba takwa hilo halipo kisheria,

Aidha amesema kua wazazi wengi wamekua wakiwafungia watoto ndani na huo ni ukatili wa kijinsia.

Sauti ya afisa ustawi

Bw. Girigit ameendelea kwa kusema watoto wengi wamekua wakifanyiwa ukatili wa kijinsia na kupelekea mtoto kuathirika kisaikolojia kwa kuogopa kuwaawambia wazazi wao kutokana na  kukosekana kwa mawasliano mazuri kati ya mtoto na mzazi.

Sauti ya Afisa ustawi