Je, unaijua hatari ya kuchoka kwa bana ya jiko lako?
4 June 2024, 2:03 pm
Matumizi ya jiko la gesi lenye bana iliyochoka inaweza kusababisha gesi kuvuja na kusambaa ndani ya chumba au nyumba kama mtumiaji akiwasha bila kuacha nafasi ya gesi kuondoka inaweza kusababisha moto kuwaka.
Na Hamisi Makungu
Jamii imetakiwa kuzingatia matumizi salama ya nishati ya gesi ili kuzuia uwezekamo wa kutokea kwa mlipo wa moto unaoweza kusababisha madhara katika jamii
Wito huo umetolewa na mwakilishi kutoka jeshi la zimamoto mkoa wa Tanga Staff Sajent Musaa Msengi wakati wa mafunzo yaliyotolewa kwa wafanyakazi wa shirika la Uzima Kwa Sanaa(UZIKWASA)
Pia ameongelea umuhimu wa kubadilisha banner za kwenye gesi ndogo kwa kuwa zikitumika kwa muda mrefu uweka matundu ambayo husababisha kuharibu mpangilio wa utokaji wa gesi kwenye mtungi wake.