Marufuku kutumia viti vya Wanafunzi kwenye Mikutano ya Vijiji Pangani.
18 January 2021, 12:37 pm
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga imepiga Marufuku Matumizi yaViti na Madawati ya Shule kwenye Mikutano ya Viijiji.
Katazo hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bwana Isaya Mbenje wakati akizungumza na Kituo hiki, ambapo amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya kutumiwa kwa viti vya Wanafunzi katika Mikutano ya Wananchi inayofanyika kwenye maeneo ya Shuleni, hivyo amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kusimamia agizo hilo.
“Vile viti, meza au Madawati ya Shule yametengenezwa kulingana na uzito wa kiwango cha Wanafunzi, sasa kumekuwa na Tabia ya Mikutano ya Vijiji kufanyika kwenye maeneo ya shule, utaratibu huu unaharibu, kwa hiyo walimu wanabeba viti na kupeleka kwenye mikutano ya Wananchi, viti vile vikikaliwa na watu wa zima kama mimi zaidi ya mara tatu kwa vyovyote vile vitaharibika”.Amesema Mkurugenzi huyo na kuongeza kuwa “Zaidi Utaratibu na watendaji Napiga marufuku matumizi ya viti vya shule kwenye mikutano ya wananchi, na watendaji wangu wa kata na vijiji nimewaagiza kusimamia hili kuhakikisha kwamba mikutano ya wananchi inafanyika kwenye maeneo ambayo haitalazimika kutumia viti na meza za shule au madawati kwa shule za msingi”
Amesema Bwana Isaya Mbenje
Hata hivyo Bwana Mbenje amewataka Walimu kuhakikisha wanasimamia na kuitunza vizuri Miundombinu ya Shule ikiwemo Viti na Madawati ya Wanafunzi hata ikiwa havitumiwi kwa wakati huo.
“Wito wangu kwenu Walimu mhakikishe viti vyote vinatunzwa vizuri hata kama kiti hakitumiki kwa kipindi Fulani kitunzwe mahali sahihi, mpaka tarehe 30 mwezi huu wa January nataka kujua kila shule ina viti vingapi, vingapi vinatumika na vingapi havina matumizi”
Amesema Bwana Mbenje